Genesis 22:20-23

20 aBaada ya muda, Ibrahimu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: 21 bUsi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), 22 cKesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” 23 dBethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Ibrahimu hao wana wanane.
Copyright information for SwhKC